Ikumbukwe kuwa Lowassa yupo katika adhabu ya
kutoshiriki katika masuala yoyote yahusianayo na kampeni za chinichini
za urais, baada ya kamati ya maadili ya CCM)kutoa hukumu yake mwezi
uliopita.Waziri Mkuu
aliyejiuzulu, Edward Lowassa amekerwa na tabia ya baadhi ya watu
wanaosambaza uzushi katika mitandao ya kijamii kwa kutumia jina lake.
Lowassa alisema kuna watu wanaoendeleza kusambasa
picha ya noti ya Sh500 yenye picha yake huku wakiongeza maneno mabaya
juu yake.
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake, Lowassa
alisema, “Kitendo hicho siyo utani, bali ni dhihaka na dharau kwa alama
za Taifa na mamlaka ya nchi.”
“Hizi ni alama za Taifa ambazo zinatakiwa kulindwa
na kuheshimiwa na watu wote, si busara kwa hao wanaozichezea kuendelea
kufanya hivyo, kwani ni dharau kubwa kwa Taifa’ alisema.
Katika noti hiyo ya Sh500 inaonekana upande wa
kulia wa noti hiyo picha ya Edward Lowassa, huku ikikaribiana na ngao ya
Taifa huku ikionyesha kuwa ilitolewa na Benki Kuu ya Tanzania..
Alisema anaheshimu maoni ya watu na nguvu ya
mitandao ya kijamii, lakini anasisitiza umuhimu kwa wananchi hao kutumia
nguvu hiyo ya mitandao kwa kujadili maendeleo ya nchi badala ya kuzusha
mambo yasiyo na tija. Kwa nyakati tofauti, picha hiyo imekuwa ikisambaa
katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo ya Facebook, Instagram,
Whatsapp, na Twitter huku kukiwa na maneno kama “timu Lowassa” na
mengineyo.
Ikumbukwe kuwa Lowassa yupo katika adhabu ya
kutoshiriki katika masuala yoyote yahusianayo na kampeni za chinichini
za urais, baada ya kamati ya maadili ya CCM)kutoa hukumu yake mwezi
uliopita.
Adhabu hiyo pia iliwakumba wengine watano wakiwamo
Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
(Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira, Naibu Waziri wa Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia, January Makamba na aliyewahi kuwa Waziri wa
Nishati na Madini, William Ngeleja.
Moja ya sababu ya adhabu hiyo ya miezi 12 ilikuwa
ni kuanzisha kampeni za chinichini za kugombea urais mwaka ujao nje ya
muda uliopangwa, ambapo baadhi ya wanachama akiwamo Lowassa walituhumiwa
kuhusika kuandaa makundi na fulana za kujinadi.
-Mwananchi
-Mwananchi
Post a Comment