Featured

    Featured Posts

Loading...

JOHARI AWARUSHA ROHO RAY, CHUCHU!

Johari.
WATU bwana! Picha zilizosambaa mitandaoni zikimuonesha staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ akiwa kwenye pozi tata na Ostaz Juma Namusoma zimetafsiriwa kuwa zililenga kuwarusha roho wapendanao; Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans.Hiyo imekuja baada ya kuvuja habari za Ray kumpangia Chuchu nyumba ya gharama maeneo ya Mwananyamala jijini Dar hivyo Johari ambaye inaaminika kuwa alikuwa mpenzi wa Ray, aliamua kuziachia picha hizo zinazomuonesha akiwa na bosi huyo wa Mtanashati Entertainment ili kumrusha roho Ray.

Ray.
Picha hizo zilisindikizwa na maneno ambayo yalionesha dhahiri kuwa Ostaz ni mtu ambaye amempa Johari msaada mkubwa maishani.
“Huyu (Johari) ni mmoja wa wanawake ambao hatanisahau katika maisha yake, siri ninayo mimi, sijui ninyi mtafikiria nini?” aliandika Ostaz ndipo wachangiaji wakaanza kutiririka:

Chuchu.
“Johari safi sana, kama mbwaimbwai tu, tupia tu picha zozote maana hakuna anayekufunga kama ni huyo Ray, mapenzi yalishakwisha zamani…” mmoja wa mashabiki wake alichangia mtandaoni huku akiungwa mkono na wengine.
Paparazi wetu alipounasa mchongo huo, alimvutia waya Johari kumuuliza kama kweli alifanya hivyo kwa nia ya kumrusha roho Ray na Chuchu lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
Chuchu na Ray katika pozi.
Kabla ya penzi hilo motomoto na Chuchu, kwa nyakati tofauti Ray amewahi kuripotiwa kuwa anabanjuka na Johari pamoja na mwigizaji Ruth Suka ‘Mainda’.
-CHANZO: TUANGAZE BONGO 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright SINGIDA KWETU
Back To Top