Naibu Waziri Tamisemi(Elimu)Kassim Majaliwa akikagua Ukarabati unaondelea katika shule ya wasichana Masasi alipokuwa katika ziara ya siku tatu mkoani Mtwara
Naibu waziri wa Tamisemi akikagua Miradi ya Ujenzi katika baadhi ya shule za Sekondari wilayani Nanyumbu
Na Abdulaziz Video,Masasi
Walimu wa shule za msingi na sekondari nchini wanaidai serikali zaidi ya Tsh. Bilioni 61.4 ikiwa ni madai ya malimbikizo ya mishahara, likizo,uhamisho,matibabu pamoja na masomo.
Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa elimu Tamisemi Kasimu Majaliwa wakati anazungumza na walimu wa shule za sekondari na msingi za wilaya ya masasi mkoani mtwara ambapo amekiri kwamba serikali inatambua kuwepo kwa madai hayo.
Kwa mujibu wa Majaliwa alisema kwamba kwa muda wa miaka miwili mfululizo serikali imekuwa ikihakiki madai ya walimu hapa nchini na wamebaini kuwepo kwa kundi kubwa la walimu wanaoidai serikali mazingira yanayopunguza morali ya kufanya kazi.
Amefafanua kwa kusema kwamba Kuanzia mwezi Agosti 2013 hadi Januari 2014 kiasi cha shilingi 14,743,417,936.67 kimelipwa kwa Walimu 20,839 walio katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini yakiwa ni malipo ya malimbikizo ya mishahara,uhamisho,nauli,masomo pamoja na matibabu kupitia kwenye akaunti ya mshahara ya mwalimu husika.
Majaliwa alisema kwamba Serikali bado inaendelea kukamilisha zoezi la kuhakiki madai ya walimu kupitia Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Hesabu za Serikali Zoezi ambalo limekuwa likiendelea vizuri.
Alisema kupitia uhakiki huo madai yanayofikia Tsh. 61,735,527,943 yaliwasilishwa ambapo Malimbikizo ya mishahara ni Tsh. 44,176,603,628 (Msingi Tsh. 30,131,881,918 na Sekondari Shilingi 14,044,721,586). Madai yasiyo ya Mishahara ni Tsh. 17,558,924,315 ( Msingi Tsh. 10,165,226,729 na sekondari Tsh. 7,393,697,586.00).
Awali wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya walimu hao walisema kwamba kwa muda wa miaka miwili serikali imekuwa ikihakiki madai yao hapa nchini lakini hadi leo hakuna aliyelipwa mazingira ambayo huchangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.
Post a Comment