MWANADADA anayefanya poa katika tasnia ya filamu za Kibongo Salma Jabu ‘Nisha’ hivi karibuni alilazimika kuwachezea wanafunzi waliomtaka kufanya hivyo wakati wao wakimuimbia katika maeneo ya Posta, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili, Nisha alisema aliteremka kwenye gari kwa ajili ya kuuliza sehemu aliyokuwa anataka kwenda, ghafla wakajitokeza vijana hao ambao ni mashabiki wake waliomtaka akate kiu yao.
“Ile kushuka ili niulizie sehemu nikashangaa kundi la wanafunzi limenivamia na kuanza kuniambia Nisha shuka huku wakiimba na kunitaka niwachezee, ikanibidi nifanye wanavyotaka baada ya hapo wakanielekeza nikaondoka, kiukweli nilifurahi na napenda sana kuona mashabiki zangu wakinipa sapoti,” alisema.
Post a Comment