Jambazi mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan Abdallah alimaarufu kwa jina la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa Moivo ameuwawa baada ya kupigwa risasi katika majibizano na askari wa jeshi la polisi.
Kamanda wa polisi akionyesha moja ya kifaa cha kufanyia tageti kabla ya kupiga kijulikanacho kwa jina la Glock Fab Defence moja ambacho jambazi hilo lilikuwa likitumia.
Jambazi mmoja aliefahamika kwa jina la Ramathan Abdallah alimaarufu kwa jina la Ramadhani Ndonga (37) mkazi wa Moivo ameuwawa baada ya kupigwa risasi katika majibizano na askari wa jeshi la polisi.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas Alisema kuwa tukio hilo limetokea October 10 mwaka huu majira ya saa nane na dakika nne usiku katika kijiji cha Moivo kilichopo ndani ya kitongoji cha Enaboishu wilayani Arumeru.
Alisema kuwa marehemu Ramadhan Abdallh aliuwa anatafutwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi kwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu ambayo yameshawahi kutokea ndani ya mkoa huu pamoja na katika maeneo mbalimbali ya nchi hiii.
Alibainisha kuwa kuuwawa kwa jambazi hili kumetokana na juhudi na kutumia mbinu za kisasa za kiupelelezi na kufika nyumbani kwa mtuhumiwa (marehemu) ambapo askari polisi walimwamuru ajisalimishe lakini alikaidi amri na kuanza kuwarushia risasi hali ambayo ilisababisha askari kujibu mashambulizi na kumsababishia umauti kumfika.
“Mara baada yakupiga jambazi huyo polisi walianza kumpekuwa mwili wa marehemu na alipatiana akiwa ba bastola aina ya Glock 19 yenye namba RLU976 iliotengenezwa nchini Austria ikiwa na magazine yenye risasi (14) ambapo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano yarisasi na mbali na hapo polisi pia walifanya upekuzi katika chumba cha jambazi hilo na kukuta magazine ingine moja yenye risasi (15) na magazine zingine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini kila moja ,Radio call moja yeye nembo ya ITSS/UNICTR pamoja na pikipiki aina ya toyo power king rangi nyekundu yenye namba za usajili T507 BSU pamoja na kofia ngumu”alisema Sabas
Aidha alibainisha kuwa pia katika upekuzi huo wa ndani ya nyumba ya jambazi hilo pia walifanikiwa kupata pingu moja ,plate namba ingine ya pikipiki yenye namba za usajili T 805 CVD ambapo alibainisha kuwa jambazi hili lilikuwa likibadilisha plate namba ya pikipiki kila mara pamoja na chomba maalumu cha kuwekea magazine pamoja na kufanyia tageti kabla yakupiga risasi (Glock Fab Defense moja),kifaa cha kusafishia bastola pamoja na koti kubwa jeusi.
Kamanda Sabas alitaja baadhi ya matukio ambayo jambazi hili lilishayafanya kuwa ni pamoja na tukio lililotekea Augast 6 majira ya saa tatu na nusu usiku maeneo ya kwa iddi ambapo mtuhumiwa akiwa na mwenzake ambaye ajakamatwa walimpiga risasi ya shingo mwanamke aliyefahamika kwa jina la Shamimu Rashid aliyekuwa mkazi wa sakina wakati akijiandaa kuingina nyumbani kwake ,huku tukio lingine likiwa limetokea Augast 21 saa 19:00 maeneo ya olasiti ambapo jambazi huyo akiwa na mwenzake kwenye pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi ya domo na kutokea kichwani mototo aitwaye Christen NIckson mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na kisha kufanikiwa kumpora TSH 2000 na baadae majeruhi kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.
Kamanda sabas alitumia nafasi hiyo kuwapongeza askari wake kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuwahaidi wananchi kuendelea kufanya uchunguzi na kuwabaini wahalifu wote na kuwachukulia sheria kali.
“arusha sio sehemu ya kuifadhi wahalifu ivyo tutajitaidi kwa hali na mali kuhakikisha tunawamaliza majambazi wote pamoja na wahalifu wote na napenda kuwaaambia wahalifu waache mapema maana sasa ivi tumejipanga vilivyo ,pia napenda kuchukuwa nafasi hii kuwaomba wananchi pia waendelee kuwafichua wahalifu popote pale ili tuwaangamize kabisa”alisema Sabas
Mmoja wa wananchi ambaye alijitokeza kushuhudia maiti ya jambazi hilo Aliyejitambulisha kwa jina la Alaija Saro akiongea na libeneke blog hili alilipongeza jeshi la polisi kwa kuweza kumuangamiza jambazi hilo kwani limekuwa likiwatia mashaka watu wengi na kuwanyima raha kwa jinsi walivyokuwa wanauwa watu.
Post a Comment