Wananchi wajitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza mjumbe wa halmasahuri kuu taifa.mh hassan mazala aongea na wananchi na kusisitiza vijana kujitambua na kuwa na imani na chama cha mapinduzi asisitiza vijana kutodanganyika na vyama vingine kwani chama cha mapinduzi ndo chama chenye nguvu na haki kuliko vyama vyote
akiwa katika miradi hiyo alitembelea maabara ya shule ya sekondari utemini,shule ya sekondari mitunduruni pia shule ya msingi ya utemin na kukagua mradi wa vyoo vya kisasa pia na kuzindua mashina mbali mbali na kugawa kadi kwa wanachama wapya akiongea katika semina mbali mbali katika kata hizo alisisitiza wanaccm kuwa na umoja na kuwa na uzalendo juu ya wagombea watakaosimamishwa na chama cha mapinduzi,asisitiza kila mwanachama ana haki ya kupiga kura na kila kiongozi anatakiwa ahakikishe ccm inashinda.mwisho asema kuna maneno maneno yanaelea juu juu ukimuuliza mtu anasema amesikia kwamba mbunge wa jimbo la singida mjini hatagombea huo ni uongo na uzushi na anaezusha hayo ashindwe,ni kwamba mohamedi ghulam dewj atagombea na kwa ridhaa ya wana singida ataendelea kuwa mbunge wa jimbo la singida mjini.
-HABARI NA MWANDISHI WA MO TV DSAMMY
Post a Comment