WAKATI siku zikishika kasi kuelekea uchaguzi mkuu mwakani,’Bundi’ ametua ndani ya CHADEMA mkoa wa Singida na hali imechafuka kwa viongizi wake kuanza kuvuana uanachama na kufukuzana uongozi.
Baraza la uongozi mkoa wa Singida, limemvua na kumfukuza uongozi Mwenyekiti wa jimbo la Singida mjini,John Kalaye Kumalija kwa tuhuma ya kuwa na mgogoro wa muda mrefu na katibu wake.
Uamuzi huo umeaanza kutekelezwa kuanzia Oktoba saba mwaka huu.
Hayo yamo kwenye barua iliyoandikwa na Katibu baraza la uongozi mkoa wa Singida,Patrick Mssuta ya Oktoba saba mwaka huu, isiyokuwa na kumbukumbu.
Aidha,kwa mujibu wa baraua hiyo, inadai Mwenyekiti huyo alifanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kugombana hadharani na Katibu wake Yahaya Ramadhan.
Kutokana na uamuzi huo,baraza la uongozi mkoa wa Singida limemwagiza Kumalijakukabidhi ofisi mara moja kwa katibu mwenezi wa jimbo,mwenyekiti wa baraza la wazee au kamati ya utendaji ya jimbo.
Hata hivyo,Katibu Mssuta katika barua yake hiyo, amejichanganya baada ya kichwa cha habari kusomeka kuwa Kumalija anasimamishwa uongozi, halafu ndani ya maelezo yake amesema baraza la uongozi mkoa,limemvua na kumfukuza uongozi.
Kwa upande wake Kumalija amejibu mapigo kwa barua yake ya Oktoba 31 mwaka huu ambayo nayo haina kumbukumbu.
Katika barua yake,Kumalija amedai kuwa hana mgogoro wowote na katibu wake Yahaya Ramadhan.
“Kwa sababu hizo na zingine,Mimi John Kalaye Kumalija,najitambua kuwa bado ni mwenyekiti halali wa CHADEMA jimbo la Singida mjini”.
Post a Comment