Ndoa tamu! Mkongwe wa sinema za Kibongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amesema kuwa, wasanii wa kike wamekuwa wakimpa usumbufu kiasi cha kuifanya ndoa yake itetereke kutokana na kuvutiwa naye kimapenzi.
Pasipo kuwataja majina, Mzee Majuto alisema mastaa hao wamekuwa wakimsumbua kiasi cha kusababisha kero kubwa kwa mkewe na kumfanya apoteze imani kwenye ndoa yake.
“Usumbufu upo wala siwezi kuwalaumu sababu mimi japo ni mzee lakini ni mwanaume mzuri ambaye ninawavutia kutokana na mambo yangu ninayoyafanya, kimsingi wanachotakiwa kuheshimu ni ndoa yangu,” alisema Mzee Majuto.
Post a Comment