Featured

    Featured Posts

Loading...

VANESSA MDEE AWEKA WAZI FITINA ZA MUZIKI NCHINI



Mwanamuziki wa kike, Vanessa Mdee maarufu kwa jina la Vee Money, amewataka wasanii kujituma katika kazi na kuachana na fikra hasi anazoamini ni kikwazo kwa walio wengi. 

Vee Money, aliyeonekana kwenye shoo ya Kourtney And Khloe Take The Hamptons (The Kardashians) inayoonyeshwa na kituo cha E! Entertainment cha Marekani, wikiendi iliyopita aliliambia gazeti hili kuwa wengi huathirika kisaikolojia kutokana na mawazo hasi wanayokuwa nayo hasa wanapokutana na changamoto ambazo ni za kawaida katika utafutaji. 

“Walio wengi hupata fikra hasi hasa wanapokumbana na changamoto. Ijulikane kwamba hakuna anayefanya kazi bila kupata vikwazo, hakuna kazi nyepesi. Sasa wakikumbana nazo wanaamini kwamba kuna fitina za mtu au watu,” alisema msanii huyo anayetamba na wimbo wake wa “Hamjui”. Akielezea mtazamo wake katika hilo, Vee Money alisema haamini kama kuna fitina katika muziki na katu hawezi kupoteza muda kufikiria mambo kama hayo. 


“Sina imani hizo na hata kama ikija kunitokea sitaamini bali nitajua ni sehemu ya changamoto za kikazi au maisha kisha nitasonga mbele. Unajua tunapoteza muda kwa kuwa na imani potofu, hata kama fitna zitakuwepo onyesha uwezo wako usikubali zikupoteze,” alisema. Alisema wasanii wengi hupotea kutokana na kuamini nguvu ya fitna na mwisho wa siku wanashuka kimuziki. “Wengi wanashuka kimuziki kwa kukosa plan B, japokuwa wengine hulewa sifa na kutokuwa na usimamizi mzuri ni moja ya sababu pia,” alisema Vee Money
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright SINGIDA KWETU
Back To Top