Featured

    Featured Posts

Loading...

AUDIO: LARK MARSH FT SAJNA - TUNDA LANGU

 
Msanii wa Bongo Fleva toka mkoani Singida Lark Marsh kwa Kushirikiana Mkali wa bongo Fleva Sajina waja na nyimbo mpya ijulikanayo kwa jina la Tunda Langu

BOFYA HAPO CHINI KUSIKILIZA NYIMBO

VODACOM YAWEZESHA SEMINA YA DARAJA LA MAFANIKIO KWA VIJANA‏

Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (wa pili kutoka kulia) akifuatilia semina ya Daraja la Mafanikio iliyoandaliwa na American Chamber of Commerce (AMCHAM) kwa udhamini wa Vodacom Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kupitia semina hiyo, mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali (pichani) walipatiwa ujuzi wa jinsi ya kuandika CV, barua za maombi ya kazi pamoja na ujuzi utakaowasaidia kutafuta kazi katika makampuni makubwa na yale ya kimataifa.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (kushoto) akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya American Chamber of Commerce (AMCHAM) Bakhti Shah alipohudhuria semina ya Daraja la Mafanikio iliyoandaliwa AMCHAM  kwa udhamini wa Vodacom Tanzania jijini Dar es Salaam leo. Kupitia semina hiyo, mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali (pichani) walipatiwa ujuzi wa jinsi ya kuandika CV, barua za maombi ya kazi pamoja na ujuzi utakaowasaidia kutafuta kazi katika makampuni makubwa na yale ya kimataifa. Kulia ni Mkurugenzi wa Compass Communication Maria Sarungi Teshai.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akifafanua  jambo wakati wa semina ya Daraja la Mafanikio iliyoandaliwa na American Chamber of Commerce (AMCHAM) kwa udhamini wa Vodacom Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kupitia semina hiyo, mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali (pichani) walipatiwa ujuzi wa jinsi ya kuandika CV, barua za maombi ya kazi pamoja na ujuzi utakaowasaidia kutafuta kazi katika makampuni makubwa na yale ya kimataifa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Empower, Miranda Naiman na kulia ni Mkurugenzi wa Kazi Services, Zuhura Muro.

MWIGULU NCHEMBA AUTEKA MJI WA GEITA

Mwigulu Nchemba akiwasili Uwanja wa MKutano Geita mjini jana.
Comrade Mwigulu Nchemba mbaye ni Naibu katibu Mkuu CCM Bara akionesha Ishara ya Dole "Mambo Poa" wakati akiwasalimia wananchi wa geita hii jana.
Mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Mwigulu Nchemba yakiendelea kwa shamrashamra za kutosha.
Hisia za Wananchi kwa Mwigulu Nchemba ambaye katika Bango moja wapo anasomeka kama SOKOINE WA PILI NCHINI TANZANIA.
Sehemu ndogo tu ya Maelfu ya Wananchi waliofika Kumsikiliza Mwigulu Nchemba.
Mwigulu akikaribishwa Geita kwa Mabango.
Kiongozi wa ACT Kanda ya Ziwa(Mratibu) akitoa shukrani zake za dhati kwa Mwigulu Nchemba kwa namna alivyokuwa mfano kwa kutetea Masikini na Wanyonge ndani ya BUnge na Nje ya Bunge.
Mkuu wa Mkoa wa Geita akisalimia wananchi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Msukuma akizungumza na Wananchi wake kuhusu Kero mbalimbali zinazowakumba ndani ya Mkoa wa Geita,Kubwa likiwa Wazawa kutopewa kipaumbele kwenye Madini, Pia unyanyasaji kwa Wachimbaji wadogo.
Comrade Mwigulu Nchemba wakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita wakati wa Mkutano jana.
Tanzania Oyeeeeee,Hiyo ndio salamu ya Mwigulu Nchemba mara zote apandapo Jukwaani kuzungumza na Wananchi.
"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hatujazi nafasi,Tunatafuta viongozi wenye uwezo wa kusimamia Halmashauri zetu za Vijiji, Mitaa na Vitongoji ili ziweze kufanya kazi za Maendeleo kwa Uadilifu na Ufanisi wa hali ya Kuridhisha"
Hii ni sehemu tu ya Maelfu ya Wananchi wa Geita waliofika Kusikiliza Ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mwigulu Nchemba,Kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Kero za Wananchi wa Geita.
Mwigulu Nchemba akiwasisitiza Wananchi kuchagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi kwasababu ndio wenye sera inayotekelezwa,Hivyo wanajua mahitaji ya Wananchi wao.
"Kuna Wananchi wanatamani sana kubadirisha Vyama kama Nguo,Kubadirisha vyama sio suluhisho la Kutatua kero za Maendeleo.Tujitahidi kufanya maamuzi yenye tija wakati wa uchaguzi,tuchague Viongozi imara na wenye nia ya kuwaongoza.Achaneni na kubadirisha vyama vya siasa"
Kupanga ni Kuchagua
Naibu katibu Mkuu akisisitiza kuwa hakuna atakaye ichafua Tanzania yeye akabaki salama,Hakuna atakaye Iba mali ya Umma akatembea kifua mbele.Wahujumu Uchumi wote wa Nchi hii waanze kujiandaa kisaikolojia.
Muonekano wa Umati wa Wananchi waliotulia wakisikiliza hoja za Msingi kutoka kwa Mwigulu Nchemba.
Comrade Mwigulu Nchemba akisisitiza Jambo kwa Wananchi wa Geita Mjini kuhusu Uchaguzi wa serikali za Mitaa.
Sehemu ya Wananchi wakati wa Mkutano huo.
Comrade Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Geita Mjini.
MKutano Umeshamalizika na Wananchi wanarejea makwao.

JK APIGA TIZI MARA TATU KWA SIKU KUIMARISHA AFYA YAKE

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazoezi leo katika viwanja vya Ikulu kufuatia ushauri wa madaktari waliomtaka afanye hivyo mara tatu kwa siku ili 

kuendelea kuimarisha afya yake baada ya kufanyiwa upasuaji mwezi uliopita katika hospitali ya Johns Hopkins nchini Marekani. 
(Picha na Ikulu)

DIAMOND AWASILI WASHINGTON, DC TAYARI KWA MAKAMUZI YA SHEREHE YA UHURU

 Diamond akiwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa Dulles muda huu tayari kwa makamuzi ya sharehe ya Uhuru itayofanyika muda si mrefu Sheraton, ya Downtown Silver Spring, Maryland.
 Diamond akimsalimia mwenyeji wake hayupo pichani mara tu alipowasili Dulles.
 Kutoka kushoto ni Dj Romy Jones, Diamond na mmoja wa waratibu wa sherehe ya Uhuru Bwn. Phanuel Ligate

MSANII LARK MARSH AACHIA VIDEO YAKE MPYA FOREVER


 

BOFYA PLAY HAPO CHINI KUANGALI HIYO VIDEO HIYO

SIKILIZA NA KU DOWNLOAD NYIMBO MPYA YA MSANII LARK MARSH FT K FAN NA LOGGIC - MANENO YENU




Msanii lark marsh, ameachia nyimbo mpya ya audio inaitwa maneneo yenu, bofya hapo chini kusikiliza na ku download hiyo nyimbo 

BOFYA PLAY HAPO CHINI KUSIKILIZA HIYO NYIMBO

DIAMOND, MAMA’KE, ZARI WALA BATA SAUZ

GOOD time! Katika hali ya kushangaza, mkali wao ndani ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, mama’ke (Sanura Kassim ‘Sandra’) na mama la mama, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ wamekutana pande za Sauz na kuponda raha, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo.
Mkali wao ndani ya Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akila bata na mtoto mzuri, ‘Zari The Boss Lady’.
Chanzo makini kilicho karibu na Diamond, kimeeleza kuwa msanii huyo na mama’ke, katikati ya wiki iliyopita, walikwea ‘pipa’ kwenda nchini humo kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kuhudhuria ‘event’ ya utoaji Tuzo za Channel O (Choamva) ambazo msanii huyo ameshiriki.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Zari wkiwa kwenye picha ya pamoja na Kampani waliyokuwa nayo Sauzi.
Kwenye tuzo hizo, Diamond ameingia katika vipengele vinne tofauti; Video Bora ya Mwaka, Mwanamuziki Bora Chipukizi, Mwanamuziki Bora wa Afro Pop na Mwanamuziki Bora wa Afrika Mashariki.
Chanzo hicho kilisema pamoja na event ya tuzo hizo, Diamond atatumia muda huo kukutana na mtoto mzuri Zari ambaye ndiye anayedaiwa kurithi mikoba ya aliyekuwa mpenzi wake, Wema Sepetu ‘Madam’ waliyemwagana hivi karibuni.
Nasibu Abdul ‘Diamond’ akipozi na mama’ke (Sanura Kassim ‘Sandra’).
“Diamond ameona bora aondoke na mama’ke wakale bata lakini pia watakutana na wifi Zari si unajua tena ndiyo kwanza mahaba niue…project zinaendelea Sauz,” kilisema chanzo hicho makini.

Gazeti hili lilifanya jitihada za kuwasiliana na Diamond ambaye pia aliambatana na dada’ke wa hiyari, Halima Kimwana lakini hakuwa tayari kuzungumzia chochote juu ya ukaribu wake na Zari zaidi ya kuanika picha zilizomuonesha akiponda raha.

MZEE MAJUTO: MASTAA WA KIKE WANATAKA KUNIVUNJIA NDOA YANGU!

Ndoa tamu! Mkongwe wa sinema za Kibongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’  amesema kuwa, wasanii wa kike wamekuwa wakimpa usumbufu kiasi cha kuifanya ndoa yake itetereke kutokana na kuvutiwa naye kimapenzi.
Mkongwe wa sinema za Kibongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ akiwa na Sabby.
Pasipo kuwataja majina, Mzee Majuto alisema mastaa hao wamekuwa wakimsumbua kiasi cha kusababisha kero kubwa kwa mkewe na kumfanya apoteze imani kwenye ndoa yake.
“Usumbufu upo wala siwezi kuwalaumu sababu mimi japo ni mzee lakini ni mwanaume mzuri ambaye ninawavutia kutokana na mambo yangu ninayoyafanya, kimsingi wanachotakiwa kuheshimu ni ndoa yangu,” alisema Mzee Majuto.

WASTARA AKANA KUCHUMBIWA


STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma, amepinga vikali taarifa kuwa ametolewa posa na msanii mwenzake, Bond Bin Sinan  na kusema kuwa kwa sasa hahitaji kuchumbiwa, wala bwana kwani hajaamua kwenda huko.
Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma.
Akikitendea haki kipaza sauti cha Ijumaa Wikienda, Wastara alisema anaona kuwa aliyeeneza habari hizo anamuwangia kwani hana wazo la kuchumbiwa kwa sasa.
“Sitaki kuolewa wala kuchumbiwa, wala bwana bado sijaamua kwenda huko,” alisema Wastara ambaye amekuwa akipinga vikali kuwa na uhusiano Bond licha ya kuonekana naye kwenye pozi tata mara kwa mara.

AJARI: BASI LA HAPPY NATION LAPATA AJARI



Watu 37 wamejeruhiwa mara baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka mkoani Mbeya kwenda Dar es salaam kupasuka tairi na kupinduka katika eneo la Meta wakati dereva akifanya jitihada za kuikwepa baiskeli katikati ya barabara, Chimala, Mbarali mbeya. Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Happy Nation lenye namba za usajili T. 281 ARR Scania lililokuwa likendeshwa na dereva aliyefamika kwa jina moja la Shabani.Taarifa 



iliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi inasema kuwa basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea mkoani Dar es Salaam. Amesema ajali hiyo imetokea leo Nov 7 majira ya asubuhi baada ya kupasuka tairi la mbele kushoto hali ambayo ilisababisha kuacha njia na kupinduka.
Amesema mara baada ya kupasuka tairi dereva alishindwa kuimudu nahasa kutokana na eneo lenyewe kuwa na kona kali hivyo aliamua kuligongesha kwenye ukingo wa barabara nakusabisha hali hiyo.


Aidha Msangi amesema kuwa kati ya majeruhi hao 29 ni wanaume na wengine 8 nakwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
Amesema kuwa majuruhi Sita kati ya wote hali zao ni mbaya na tayari wamefikishwa katika hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi wakati majeruhi wengine 10 wakiwa wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya Chimala.


Akithibitisha kupokea kkwa majeruhi hao Muuguzi katika chumba cha msaada wa haraka hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt Orivia Masoi amesema kuwa wamepokea majeruhi sita ambapo wanne wamelazwa wodini na wawili tayari wameruhusiwa.
Aidha mmoja wa majeruhi Nicolaus Fungo ambaye amelelazwa wodi namba moja kwa ajili ya matibu hao amesema majeraha makubwa maeneo ya mbavuni na kwamba hali yake inaendelea vizuri mara baada ya kuaptiwa matibabu.
© Copyright SINGIDA KWETU
Back To Top