KAZI sana! Mkazi wa Buguruni, Rukia Nassor amekimbilia Kituo cha Polisi Buguruni jijini Dar kutoa taarifa ya bintiye Saida Said (18) (pichani)kutoroshwa nyumbani kwake siku chache kabla ya ndoa.Alipofika kituoni hapo, mwanamke huyo alimtaja mtu mmoja kwa jina moja la Shaban kwamba ndiye aliyefanya kitendo hicho.
Akizungumza na Uwazi juzi, mmoja wa ndugu ambaye hakupenda jina lake lichapishwe gazetini alisema mama huyo amekuwa akihaha kwa binti yake kotoroshwa na mwanaume huyo tangu Septemba 25, mwaka huu ambapo kila akimpigia simu hapatikana hewani.
Jeshi la polisi bado liko ndani ya msako mkali ili kuhakikisha binti huyo anapatikana na hatua za kisheria zinachukuliwa kwa mwanaume huyo.
“Mpaka sasa mama wa bi harusi hajatoa taarifa kwa bwana harusi wala ndugu zake, amekuwa akimtafuta kimyakimya huku akimuomba Mungu binti yake apatikane kwa vile mahari alishalipwa, sasa anaogopa ikifika siku ya ndoa itakuwa aibu kubwa,” alisema ndugu huyo
Ndugu huyo alisema Saida alitarajiwa kufanyiwa ‘kitchen part’ Oktoba 31, mwaka huu na kufuatia na ndoa Novemba 6 huku ikidaiwa kuwa, upande wa bwana harusi michango inaendelea kama kawaida.
Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu; BUR/RB/10170/2014 KUTOROSHA.
Jalada la uchunguzi kuhusu kutoroshwa kwa bi harusi huyo linasomeka Kumbukumbu; BUR/RB/10170/2014 KUTOROSHA.
Post a Comment