Mtanzania Laveda Jumapili October 19 aliponea chupuchupu kwa kubaki kwenye jumba la Big Brother Africa, huku akiwashuhudia washiriki wenzake watatu wa kike wakitoka mchezoni.
Esther (Uganda) , Lilian (Nigeria) pamoja na Sabina (Kenya) ndio washiriki walioondolewa katika shindano hilo usiku wa jana ikiwa ni ‘eviction’ ya pili toka shindano lianze.
Hadi sasa washiriki watano wa kike wametoka katika shindano hilo na kufanya idadi ya washiriki wa jinsia ya kike kubaki 8 huku wanaume wakiwa 13.
Nchi za Zambia, Mozambique, Kenya, Uganda and Nigeria kila moja imeshapoteza muwakilishi mmoja hivyo zote zimebaki na muwakilishi mmoja mmoja tu mjengoni.
Post a Comment