SiKU chache baada pedeshee Mkongo, Mwami Rajabu kutangaza kuwa anamtaka staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa gharama yoyote, mwigizaji huyo ametoa jibu linaloonesha dhahiri kwamba alikuwa radhi kumkubalia.
Akizungumza na waandishi wetu mara baada ya habari ya Mkongo huyo kuandikwa gazetini hivi karibuni, Lulu alisema kilichomshangaza kutoka kwa mwanaume huyo ni kwamba hakutakiwa kuanika hisia zake katika vyombo vya habari kama kweli ana nia ya dhati, angemtafuta mwenyewe au kwenda kujitambulisha nyumbani kwao.
“Namshangaa sana huyo Mkongo kwa kweli kama angekuwa na mapenzi ya kweli asingeyaeleza kwenye magazeti, angenitafuta au angekuja nyumbani kwetu hapo ningemuona kweli ananipenda,” alisema Lulu.
Staa huyo aliendea kumwaga chache kuwa, kama mwanamke, anahitaji kupewa heshima yake na kudai kuwa wanaume wengi wa sasa wamejisahau kupindisha mila za Kiafrika kufuata taratibu na badala yake wanatanguliza fedha mbele.
“Nadhani watu wamesahau mila za Kiafrika kabisa, huwezi kuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke halafu utumie rafiki au vyombo vya habari umpate, hiyo inakuwa siyo heshima kabisa,” alisema Lulu.
Post a Comment