BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, diva wa filamu Bongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa kimya chake hicho kina mshindo kwani kuna kitu kilimuweka bize hivyo watu wakae mkao wa kula atawasapraizi.
Batuli alisema hayo baada ya mashabiki kuuliza amepotelea wapi ambapo alisema kuwa aliamua kukaa kimya kidogo ili mashabiki wapate hamu ya kumuona kwani kitu alichowaandalia kiko njiani.“Ukimya wangu una sababu kubwa, nimeamua kufanya yangu ili mwisho wa siku nikiibuka nitoke na la kunitangaza,” alisema Batuli.
Post a Comment