Kala Jeremiah amesema anatarajia kuachia wimbo mpya wa kufungia mwaka kabla mwezi huu haujaisha.
“Mwezi wa 11 hautaisha Kala Jeremiah atadrop kitu ambacho naamini kabisa kila Mtanzania kitamgusa..kwa namna moja au nyingine kila mmoja unamhusu huu wimbo kwahiyo sitaki sana akuongelea sasa hivi “ Amesema Kala kupitia Power Jams ya EA Radio. Akiuzungumzia wimbo huo, rapper huyo wa ‘Dear God’ amesema huo ndio utakua wimbo wake wa kwanza kuwatoa watu machozi katika nyimbo zake zote alizowahi kutoa.
“Kiukweli kabisa mimi sijawahi kufanya wimbo anaskiliza mtu analia ndo wimbo wangu wa kwanza mtu anaskiliza analia yaani anaskiliza tu mashahiri yale mwanzo mwa wimbo mpaka mwisho wa wimbo lakini mtu anadondosha machozi, nadhani nimefanya kitu ambacho kita wasurprise watanzania”
Post a Comment