Makonda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).…Akionyesha moja ya magazeti yaliyoandika vurugu za jana.Waandishi wa habari wakisikiliza taarifa ya Makonda (hayupo pichani).
(Patrick Bozohera na Gabriel Ng’osha/GPL)
KATIBU Mwenezi Idara ya Hamasa na Chipukizi ya
UVCCM, Paul Makonda, amekana kuhusika katika vurugu zilizotokea jana
katika mdahalo wa Katiba Iliyopendekezwa ambao ulioandaliwa na Taasisi
ya Mwalimu Nyerere chini ya Mwenyekiti wake Joseph Butiku.Hayo ameyasema leo katika hoteli ya Protea, Osterbay, jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari.
Mkutano huo ulikumbwa na vurugu wakati aliyekuwa mwenyekiti wa kuratibu katiba mpya, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha mada yake, katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Post a Comment