Tukio hili la kusikitisha limetokea Mkoani Iringa ambapo mwanamke mmoja alijifungua mtoto na kisha kumdumbukiza katika tundu la choo. Mtoto huyo alizaliwa nyumbani sio hospitali baadae siku ya tarehe 04/11/2014 mama huyo alimdumbumiza kichanga hiko jinsia ya Kiume chooni.
Mama huyo alietambulika kwa jina la Magdalena inasemekana lengo kuu la kufanya kitendo hiko cha kikatili ni kuficha ukweli kwa mume wake aliekua safarini kuwa amezaa. kwani tabia yake imekua ni kutoka na wanaume wengine pindi mumewe akiwa hayupo na this time alinasa. ili kujinasua akaamua kudumbukiza mtoto chooni na yeye abaki kuwa mwanamke kwema mbele ya macho ya mumewe.
Mtoto huyo alidumbukizwa chooni jion/usiku wa tarehe 04 na kuokolewa asubuhi yake tarehe 05/11/2014 (leo) baada ya majirani kusikia sauti za kilio cha mtoto mchanga. Mtoto huyo yuko hospitalin kwa sasa huku mama yake akishikiliwa na polisi mwa mahojiano zaidi.
Post a Comment