Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza na wanahabari jioni ya leo mara baada ya tukio hilo la kukamatwa kwa Mbunge wa CHADEMA akigawa fedha kwa wanakijiji siku moja kabla ya uchaguzi kufanyika.Uchaguzi wa Jimbo hilo unatarajiwa kufanyika kesho siku ya jumapili,ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la
Kalenga,Iringa Vijijini,Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili amekamatwa
jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini
akigawa Fedha kwa wanakijiji hao,akijua fika Wananchi hao wanatarajiwa
kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya
jumapili.
Pichani shoto ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akielekezwa
sehemu ya kupita wakati wakiondoka ofisi za makao makuu ya CCM mjini
Iringa jioni ya leo,akituhumiwa kukutwa akigawa fedha kwa Wanakijiji wa
Kitayawa kata ya Luhota,Iringa Vijijini,ambapo Wananchi hao wanatarajiwa
kupiga kura kwa ajili ya kumpata Mbunge wa jimbo hilo kesho siku ya
jumapili.
Mbunge huyo wa Chadema akipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kituo cha Polisi kwa taratibu nyingine za kisheria.
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Manyara kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA),Mh.Rose Kamili akiwa ndani ya gari ya polisi mara
baada ya kukakamatwa jioni ya leo kwenye kijiji cha Kitayawa kata ya
Luhota,Iringa Vijijini akituhumiwa kugawa Fedha kwa wanakijiji
Gari ya Polisi PT 1895 ikiondoka na mtuhumiwa huyo,mara baada ya
kuchukuliwa kwenye makao Makuu ya chama cha CCM alikokuwa ameshikiliwa
na uongozi wa chama hicho,kwa taratibu nyingine za kisheria.
Post a Comment