Mwanamke
Etina Silumba (44) mkazi wa kijiji cha Mpemba wilayani Momba
anashikiliwa na polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za kumuua mumewe.
Jeshi la polisi mkoani hapa limesema mwanamke huyo alimuua mumewe kwa kumkata kisogoni na kitu kinachosadikiwa kuwa ni panga kabla ya kumvunja shingo na mguu wa kushoto.
Jeshi la polisi mkoani hapa limesema mwanamke huyo alimuua mumewe kwa kumkata kisogoni na kitu kinachosadikiwa kuwa ni panga kabla ya kumvunja shingo na mguu wa kushoto.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Ahmed Msangi alisema mume aliyeuawa alitambulika kwa jina la Misheck Mwashiuya (52) mkazi wa Mpemba wilayani Momba.
Kamanda Msangi alisema tukio hilo lilitokea machi 10 ikiwa zimepita siku mbili tangu kuazimishwa kwa kilele cha siku ya wanawake duniani.
Alisema mwanamke huyo alitenda unyama huo kwa mumewe majira ya saa tatu usiku katika kijiji cha Ipapa kata ya Ipunga wilayani Mbozi.
Kamanda huyo alisema uchunguzi umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi na kuwa kabla ya tukio wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa kutuhumiana kuchepuka nje ya ndoa yao.
Alisema mwanamke huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilishwa na kusisitiza kwa kuwataka wanajamii kutumia njia ya mazungumzo kusuluhisha migogoro baina yao badala ya kutumia mabavu.
Post a Comment