MAAJABU! Licha ya ulimwengu wa burudani Bongo kuamini kwamba staa wa Mduara, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ aliwahi kuanguka dhambini kwa Mbongo-Fleva, Elias Barnaba, mwanadashosti huyo ameibuka na kudai kuwa hakuwahi kumpa penzi.Shilole anayetamba na Ngoma ya Nakomaa na Jiji, amefunguka hayo kupitia Global TV Online ambapo mahojiano hayo yatarushwa kwenye Mtandao wa Global leo, Jumatatu.
“Ukweli sikumpa penzi Barnaba, yule ni mshkaji tu…kama ni muziki hakunipiga tafu kama alivyonisaidia Q-Chillah …hahaha acha hizo bwana, Barnaba hakuwa mchumba wangu,” alisema Shilole.
Mbali na kumfungukia Barnaba kwenye kipindi hicho, Shilole amefunguka mambo mengi ambayo hajawahi kuyasema, hivyo ukitaka kupata uhondo zaidi, tembelea Mtandao wa Global TV Online.
-GPL
Post a Comment