Featured

    Featured Posts

Loading...

KUNDI LA VIJANA WAANZISHA VURUGU WAKATI WA MDAHALO KUHUSU KATIBA MPYA:WARIOBA AOKOLEWA NA WALINZI


Jaji Warioba akitolewa nje ya ukumbi.
VURUGU zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea hivi punde katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.



Vurugu hizo zimezuka baada ya watu waliokuwa na mabango kuvamia ukumbuni hapo na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wanafuatilia mdahalo huo kuwakabili na kuwapa kichapo.
Hali ilivyokuwa ukumbini hapo mara baada ya vurugu hizo
 Baada ya vurugu hizo, mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa moja kwa moja na ITV umesimamishwa kwa muda. 

Habari kwa hisani ya GPL na Jamii forums
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright SINGIDA KWETU
Back To Top