Vitambi
hupunguza maisha ya watu wenye hali hiyo ya afya, hivyo kusababisha
upotevu wa rasilimali-watu. Ili kuepukana na athari hiyo watu
wahakikishe wanabadili namna wanavyoishi. Wengi wana muda mchache sana
wa kutayarisha vyakula visivyo na mafuta mengi majumbani mwao, hivyo
wanakula nje zaidi, yaani kwenye hoteli na migahawa na matokeo yake ni
kuwa na vitambi. Kuna wengi wanatambua athari za tatizo la unene na
vitambi, lakini hawafanyi chochote kulirekebisha, hii inatokana na
ukweli kwamba idadi kubwa ya watu hawajui maana halisi ya kuwa na afya
njema.
Watu wengi,
hasa vijana wamekuzwa kwa kula chipsi, mikate na vyakula vya sukari na
si mbogamboga na matunda. Ukweli ni kwamba watu wengi hawafanyi mazoezi
ya kutosha kama ilivyokuwa zamani hivyo, watu wenye vitambi wanaongezeka
kila sehemu. Nchini Marekani utafiti umefanywa na kugundulika kuwa
asilimia 86 ya watu wazima nchini humo watakuwa na vitambi ifikapo mwaka
2030 iwapo hali hii ya kutozingatia masharti ya afya kuhusu unene
itaendelea, kufuatana na utafiti wa mwaka 2008 uliofanywa na mtafiti
mmoja wa Chuo Kikuu Cha John Hopkins. Ongezeko la tatizo hili la kiafya
katika nchi nyingi linatisha. Kwa ujumla, umri wa mtu mnene mwenye
kitambi huwa pungufu kwa miaka 8 hadi 10 ukilinganisha na mtu mwenye
umbo la kawaida.
Magonjwa yenye
uhusiano na kitambini moyo, aina fulani ya kisukari, magonjwa ambayo
huua mamilioni ya watu duniani kote. USHAURI Kila mtu aepuke kula
vyakula vyenye mafuta mengi na kutokula chakula kupindukia na ule
unaposikia njaa, kutotia mafuta mengi kwenye chakula na kutotumia sukari
nyingi. Kila mtu anatakiwa kufanya mazoezi ya kukimbia, kutemba au
kuogelea angalau kwa nusu saa kila siku. Watu wanashauriwa kuacha
kutumia vyakula vya kopo na hasa vile vyenye gesi nyingi. Wale ambao ni
wanene kupita kiasi waonane na daktari kwa ushauri wa kitaalamu.
Post a Comment